Mark 11:20-24

20 aAsubuhi yake walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. 21 bPetro akakumbuka na kumwambia Isa, “Rabi, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!”

22 cIsa akawajibu, “Mwaminini Mungu. 23 dAmin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng’oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa. 24 eKwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.
Copyright information for SwhKC